Genesis 13:14-17

14 aBaada ya Lutu kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. 15 bNchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 16 cNitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. 17 dOndoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”

Copyright information for SwhKC